Mureti na Mugiira wanapopata ufadhili wa kwenda kusoma katika Chuo
Kikuu cha California, Marekani wanafurahi sana.
Wanaabiri ndege kwa mara ya kwanza na wanaajabia mengi
wanayoyaona katika safari yao hadi Marekani. Lakini maajabu ya kweli
yanawasubiri California wanakokwenda kusoma. Mapokezi na mlahaka
mwema wanaopata kutoka kwa Profesa Kithaka unatiwa doa na
wasichana wawili wa Kimarekani; Mary Anne na Brigit wanaotaka
mapenzi ya lazima kutoka kwa Mureti na Mugiira.
Mary Anne na Brigit wanafanya mipango ya kuwateka Mureti na Mugiira,
kwa bastola au hata kwa mkataba (kama alivyotekwa kijana mmoja wa
Kiafrika aitwaye Mburia, kwa kulazimishwa mkataba wa mapenzi) "... kwa
siku nyingi umekuwa ukinidanganya kwamba utanioa mara mjombako
atakapokupatia kibali. Sasa chukua hii kalamu na karatasi uandike
kwamba utanioa!"
Je, Mureti na Mugiira watajinasua katika mtego wa wasichana hawa ili
kutimiza ndoto yao ya masomo huko California? Wataweza kurudi Afrika
ama watatekwa bakunja na utamaduni mpya wa Wamarekani?
Watayaacha masomo watoroke au watafanyaje?