Kizazi cha leo kimejaa una ki. Wengi wanapoajiriwa wanajidai ni
wafanyakazi waadilifu na wenye bidii kwelikweli. Kumbe wao ni
vinyonga wanaogeuza rangi ili wawasaliti mara ki na kuwaibia
waajiri wao! Hawana uaminifu wala huruma wanapotekeleza vitendo
vya ki sadi. Uadilifu, wema na utu ni misamiati migeni katika
maisha yao.
Lakini miongoni mwao kuna wachache wazuri na wenye wema.
Kwatampola analinda utu wake licha ya majaribu mengi anayopitia
kila siku. Kutokana na wema na utu wake, Kabaila Bumaali anamtunuku
Kwatampola zawadi kubwa iliyokuwa ndoto yake kila siku! Kwatampola
anasi wa kwa utu wake na kufahamika kwa makabaila wengine
sana. Ni kweli kwamba Chema Chajiuza!
Kinyume na Kwatampola, Injinia Bakehena anauza utu wake.
Anapunja pesa za mwajiri wake. Yeye ni sadi kamili wa nafsi na wa
mali. Je, Injinia Bakehena ata kwa na kitu gani mwishowe?
Ataadhibiwa ama atanusurika adhabu za waajiri wake? Je, ni
kweli kwamba 'malipo ni duniani ahera yaenda hesabu'?