Enock MaregesiEnock Abiud Maregesi alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Mwanza mnamo mwaka 1972, Novemba 25. Alisomea teknolojia ya habari na utawala wa biashara katika Chuo Kikuu cha Wales, na uandishi wa habari na vitabu katika chuo cha fasihi ya ubunifu chaThe Writers Bureau, nchini Uingereza. Alisomea pia sayansi ya roho ya Kabala katika Taasisi ya Bnei Baruch ya Petah Tikva nchini Israeli. Mnamo mwaka 2015 kitabu chake cha kwanza, Kolonia Santita: Laana ya Panthera Tigrisi, kilishinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika; iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Cornell cha New York, Marekani, na kampuni ya Mabati Rolling Mills ya Nairobi nchini Kenya. Anaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania, anakojishughulisha na biashara na uandishi wa vitabu. Read More Read Less
An OTP has been sent to your Registered Email Id:
Resend Verification Code